Maneno haya matatu huamsha hali (mizuka) ukiwa faragha la mwenzi wako, “achana na neno nakupenda”.

Kubusiana shingoni, kung’atana ng’atana kimahaba, na kutazamana. Neck kisses, nibbling and eye contact. Utafiti nchini Marekani umeonesha kuwa, maneno amabayo ni ya kawaida huweza kuamsha mizuka ya kuendelea kufanya tendo la ndoa kati yako na mwezi wako. Wamarekani 2,000 walisema kuwa kubusiana shingoni ndiyo huchochea sana hali ya kufanya mapenzi zaidi na kufuatiwa na mpenzi wako kutamka maneno ya kimapenzi.

Utafiti huo unasema kuwa, pale mpenzi wako anapotamka neno “I like that” kasi na mood ya mapenzi huongezeka zaidi na kuwa ndilo neno la pili linaloamsha ari ya kuendelea na tendo. Utafiti huo unaonesha 76% ya waliofanyiwa utafiti hupenda wapenzi wao kutokuwa kimya pale wanaposhiriki tendo na kupendelea kuwepo na mazungumzo ya chini chini.

Kuchezea masikio kwa kung’ata ng’ata kihisia ilikuwa ni sehemu ya waliofanyiwa utafiti na kuonekana kufurahia hali hiyo lakini pia kutazamana machoni wakati wa tendo ikiwa imepewa pia kipaumbele.

Mengine ni kama kunukia vizuri, kutaniana, kuchezea nywele, kuzama chumvini, mapenzi ya pupa (papara) n.k

Hashimu Rungwe azungumzia wasimamizi wa uchaguzi

“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ipo wazi kabisa (Ibara ya 74(14) kwamba wasimamizi wa uchaguzi wasijihusishe na masuala ya vyama vya siasa”

“Jimbo la Kinondoni kwenye uchaguzi wa marudio, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Aaron Kagurumjuli alikataa kutoa nakala za viapo vya mawakala kwa wakati. Uamuzi huu wa Mkurugenzi huyu ndio uliopelekea kifo cha mwanafunzi Akwelina.”

“Kwenye uchaguzi wa marudio Jimbo la Korogwe vijijini kufuatia kifo cha Mh. Stephen Ngonyani, msimamizi wa uchaguzi alitoweka ofisini kutwa nzima na kuibuka baada ya muda wa kupokea fomu kuisha na kumtangaza mgombea wa CCM, Timotheo Mzava kupita bila kupingwa”.

“Tunafahamu kwamba mapambano kwa ajili ya Tume Huru ya Uchaguzi yatafikiwa kwa kupata katiba mpya, vyama vya siasa kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia, wanaharakati, viongozi wa dini na wananchi tutaendelea kupigania katiba mpya”

“Katika zama hizi za demokrasia ya vyama vingi, haifai kuwatumia wakurugenzi ambao ni makada wa CCM halafu tukajidanganya kuwa haki itatendeka, mapenzi yao kwa CCM hayakomi baada ya kuteuliwa kuwa Wakurugenzi”

“Katika uchaguzi unaosimamiwa na Wakurugenzi makada wa CCM mpinzani hatangazwi mshindi hadi mbinu zote za kuiba kura zitaposhindikana”

“Huwezi kuwa na mfumo wa vyama vingi halafu ukawa na Katiba inayofuata misingi ya chama kimoja, ndiyo maana sisi tunasema tutaendelea kudai Katiba mpya”

“Hakuna chama tawala Afrika, watu wanajiita sisi ni chama tawala! sisi ni chama tawala! Hicho chama tawala nani amekupa? Hii inatia kichefuchefu” – Hashim Rungwe.